LIFEWATCH GROUPLtd

Jinsi Ya Kuokoa Maisha Yetu
Mission Statement: Share practical moral solutions to assure world sustainability
shida lifewatchgroup
Night Picha Inaonyesha Chini ya 40% ya Idadi ya Watu Duniani ya
suluhisho lifewatchgroup
Picha ya satelaiti ya Dunia usiku lifewatchgroup

Ukuaji wa Idadi ya Watu Duniani

Ukuaji wa idadi ya watu ulimwenguni lifewatchgroup
* The World Commission on Environment definition of sustainability: A sustainable society is one that “meets the needs of the present without compromising the ability of future generations to meet their own needs.”
haya ndio shida lifewatchgroup

MALI, NJAA NA AMANI

“Tunasafiri pamoja, katika chombo cha anga, huku tukitegemea hifadhi ya hewa na udongo; sote tunahakikisha usalama wetu kwa kudhibitisha amani na mahala pasipo na hofu; kulindwa dhidi ya uangamizi kwa kuendeleza utunzaji, bidii kazini na, nitasema, upendo tunayoipa ufundi wetu dhaifu. Hatuwezi dumisha chombo hiki kwa mbinu zilizo nusu bahati, nusu huzuni, nusu ujasiri, nusu kukata tamaa, nusu utumwa wa maadui wa kale wa binadamu, nusu huru katika ukombozi wa rasilimali zilizokuwa ndotoni pekee hadi siku hiyo. Hamna ufundi wala wafanyi kazi walioweza kusafiri kwa usalama katika utata mkubwa wa kiwango hicho. Kuishi kwetu wote unategemea utatuzi wao.” - Adlai Stevenson.

Katika safari yetu, binadamu amekosa kutii mashauri haya na sasa yumo katika njia panda iliyohitaji tuweze kubadilisha mwelekeo kwa haraka ndipo tuweze kujiokoa kabla wakati udidimie. ( 1a)(4,5).

Wakiwa katika mji wa Kairo, mwaka wa 1994, Umoja wa Mataifa ulikubali kwa kauli moja kwamba idadi kubwa sana ya watu ndio tisho kubwa zaidi ambayo watu wamekabiliana nayo (1). Mataifa mengi hawakutii maazimio ya Umoja wa Mataifa na hivyo vitisho vya binadamu na mazingira vimeongezeka na kuhitimu viwango ambavyo uwezo wa dunia kuendeleza maisha umepita mipaka (2)(29a)

Tunarufaa kwenu kama wanachama wa kizazi cha sasa wa mwananchi husika kwa sababu tunaamini ya kwamba unajali. Suluhisho la haraka ni kukuza elimu kuhusu: familia, mipango, afya, ubaguzi wa rangi, uchumi, nishati mbadala, kuhamasisha na kuwezesha wanawake na uhifadhi wa mandhari (2a) Hii itasababisha athari kubwa chanya kwa binadamu na kwa mandhari ambayo maisha yote inategemea. Tishio kubwa kwa kuwepo wetu si ugaidi, vita, au madawa ya kulevya. Tishio kubwa ni kupungua kwa maliasili na uchafuzi iliyotokana na kuongezeka kwa mahitaji ya binadamu (3).

Idadi kubwa ya watu ndiyo chanzo cha ukosefu wa ajira, njaa, uhalifu, madawa ya kulevya, ushirikiano wa familia, ugaidi na vita. Wataalam wanatabiri ya kuwa tukiendelea kuongezeka, binadamu hataweza kuishi duniani kwa miaka mia moja tusipoungana na kutatua hii shida kwa haraka (3a,3b).

Hapo zamani, katika miji na mashamba kote nchini, kazi ya mikono ilikuwa tele, iliyohitaji familia kupata watoto wengi ili waweze kusaidia kufanya kazi. Wanaume waliitunza familia, na wanawake walibaki nyumbani kulea watoto, kuhudumia wazee na wagonjwa. Waliweza kupata nafasi ya kukaa na familia yao, pahali ambapo mahitaji ya kihisia yalitimizwa. Wakati huo upendo na heshima ilikuwa kawaida, matatizo ya kisaikolojia na madawa ya kulevya yalikuwa nadra. Watu waliohitaji usaidizi waliweza kutegemea usaidizi kutoka majirani kwa sababu hisia ya huruma na jamii ilitawala..

Katika ujio wa mapinduzi wa viwanda, watu wengi walipoteza kazi baada ya uvumbuzi wa mashini, na hivyo mashindano ya ajira ilikuwa jambo la kawaida. Bidhaa zilizoweza kununuliwa na matajiri pekee wakati uliopita, ziliweza kununuliwa na watu wengi nchini kwa sababu mitambo na maliasili nyingi ilileta bei ya bidhaa chini. Biashara zilihimiza, “NUNUA. NUNUA, NUNUA!” kwa watu wote, na kuwezesha wakati wa ulaji na mashindano kati ya watu. Huu mtindo wa maisha ulihamasisha wanawake kujiunga na waliofanya kazi ili kupata riziki. Ulimwengu wetu mpya umekuwa wa mashindano na kukosa upendo, mahala ambapo wanaofaulu huishi vyema na, kwa upande mwingine, uhisani na uungwana umepungua. Kwa mfano, katika mitaa mingi, ni haramu kuwapa maskini na watu wasio na makazi vyakula na malazi (6 ,7 ).

Haya ni Dalili za Idadi Kubwa ya Watu

Dalili za idadi kubwa sana ya watu nchini zinafaa kufahamiwa ndipo tatizo hili lisuluhishwe. Leo, katika familia, waume na wake wanafika nyumbani baada ya kazi huku wamechoka kihisia na kimwili, na ndivyo huzua hoja kati yao mara nyingi; hawapati wakati wa kuwa kivyao wala wakati kuwa na familia yao. Watu wachache wanafunga ndoa sasa, na kiwango cha talaka kimeongezeka kwa miaka 50 iliyopita. Kwa mfano, nchi ya Belarus iliripoti kiwango cha talaka 50% mwaka wa 2012 (8). Mauaji ya watoto wachanga ndiyo sababu ya kwanza ya vifo vya kikatili ya watoto nchini Amerika (9,10). India ina visa vinavyoashiria kuongezeka kwa kiwango cha kujiua kwa sababu ya ukosefu wa njia za kuweza kujikimu na ajira (11).

Shinikisho linalotokana na ukosefu wa ajira linasababisha watu wengi kugeukia madawa dawa ya kulevya na pombe kama misaada. Kinyume cha hayo, Japani, nchi iliyokuwa mojawapo kati ya nchi yenye viwango vya juu zaidi vya kujiua, inaonyesha ongezeko la kiwango cha ajira tangu 2011 kutokana na kupungua kwa idadi ya watu. Kiwango cha kujiua kimeshuka, na hivyo mashindano ya ajira imepungua (12). Uchina, pamoja na sera yake ya mtoto mmoja kwa familia, ilitoka katika taifa ambalo njaa iliangamiza mamilioni ya watu, na kuwa taifa la pili tajiri zaidi duniani (13). Walakini, sera ya Uchina ya mtoto mmoja iliunda kizazi cha watu wenye ubinafsi, wanaopenda mali ambao hawana hisia ya jumuiya ambayo familia ya watoto wawili hutoa (14).

Usawa sahihi kati ya maliasili na ukubwa wa idadi ya watu yafaa kuwa ili tuweze kukuza ustawi, fursa za elimu na ajira. Kazi ndiyo chanzo cha kile ambacho kinawapa binadamu maana yao ya kusudi, hadhi na thamani. Hivi vitu ndivyo msingi wa kiuchumi na utulivu wa kijamii. Uchumi duni, kwa upande mwingine, inawezesha ugaidi, ubaguzi wa rangi na uasi inayosababisha mauaji ya kimbari au vita.(14a,14b)

Katika dunia hii ya matumizi ya bidhaa, watu hawana wakati wa kuwa na wengine, kwa hivyo ni rahisi kuwapa watu vitu vya nyenzo kuliko kuwa nao. Mwishowe, watu wa kizazi kipya wanathamini mafanikio na tuzo kwa suala la nyenzo. Si jambo la kushangaza ya kwamba uyakinifu unachukua nafasi ya mguso wa kibinadamu, ilhali hautimizi mahitaji ya kihisia. Watoto na wanandoa wanaohitaji upendo wa kibinadamu na wanaoikosa manyumbani wanaitafuta mahali pengine. Inaelezea sababu ya mimba za utotoni kufika milioni 16 ya watu wanaozaliwa kila mwaka ulimwengu mzima (15). Huko Marekani, 40% ya akina mama wapya hawajaolewa(16). Wakati huu, jamii yetu yenye msongo wa mawazo, inachora picha ya ngono kuwa mtindo mwema.

Ngono imekuwa jambo lenye wengi waliloizoea wanatafuta mapenzi na mahaba ndipo waweze kutoa msongo wa mawazo. Jambo hili lilikuwa dhahiri zaidi baada ya Vita vya Pili vya Dunia, iliyosababisha kuzaliwa kwa watoto wengi. Dhana ya kuwa vita husaidia kwa kudhibitisha kuwa ukubwa wa idadi ya watu iko sawa, ni makosa. Katika mwaka wa 1800, idadi ya watu duniani ilikuwa bilioni 1.3 na idadi ya watu huko Marekani ilikuwa milioni 5. Mwaka wa 2023, idadi ya watu duniani ni bilioni, 8.045 na idadi ya watu Marekani ni milioni 336, 704 (17).

VVita, majanga, magonjwa, na vifo vya asili, kwa upande mwingine, haijaweza kupungua ongezeko la watu. Katika mataifa maskini, familia nyingi wana watoto wengi kuliko wanavyoweza kuwakimu na kuhakikisha ya kwamba wanaishi (18). Duniani, watu wa kiasili karibu milioni 370 na watu maskini bilioni 2.6 wanaishi bila stima, maji na vifaa na kadhalika (Ona jalada la Lifewatchgroup.org’s web site - NASA NIGHT LITES) (19,20)na watu mamia ya mamilioni hawawezi kupata vyanzo salama vya maji ya kunywa (21). Watu hawa wangepata nafasi ya kuishi maisha ya kisasa kama watu walioishi kwa mataifa yaliyoendelea, ingechukua sayari tano 5 kututegemeza sisi sote (22). Kunao makabila ya watu ambao hawana mawasiliano na ulimwengu wa kisasa, ambao wana furaha na wanastawi. Hawapati matatizo ambazo ulimwengu wa sasa wanakabili. Wanafurahia maisha kwa sababu wana hisia ya jamii na heshima kwa raslimali. Hii inathibitisha ya kwamba pesa, kuishi kwa ulimwengu wa kisasa na uyakinifu sio jibu (22a).

Ustaarabu ilibadilishwa Milele na Vita vya Pili vya Dunia, Mapinduzi ya Viwanda na Kisayansi (Angalia grafu hapo juu)

Mapinduzi ya viwanda na ya kiteknolojia yanazidi kuchukua nafasi ya binadamu kupitia vyombo, tarakilishi na roboti. Watu wamelazimishwa kukosa ajira kabisa kwa namna haijawahi kuwa kwa wakati wowote uliopita na inasababisha pengo kubwa kati ya matajiri na maskini. Sheria zinazohimizi upendeleo kwa wanaadamu kuliko vifaa lazima zitekelezwe; tusipofanya hivyo hali hii itasababisha njaa, kuleta hasara, upinzani, ukatili wa polisi, ubaguzi wa rangi na ugaidi.

Historia inatufunza ya kwamba makundi ya watu wenye njaa waliangamiza miliki ya Warumi, Wafaransa na Warusi. Wakati wa sasa, bomu la wakati iliyosababishwa na kuzidi ya idadi ya watu ni uhaba wa chakula na ukosefu wa ajira, itakayowezesha matukio sawa na hayo kufanyika (23).Umaskini na kupungua kwa maliasili inasababisha watu kujidhalilisha wenyewe na kutoweza kujikimu. Kutokana na uharibifu wa mazingira, makundi ya watu wanahama kutoka nchi yao na kwenda kwa mataifa jirani, pahali ambapo wana matumaini ya kwamba watapata riziki. Hii ilisababisha ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya wageni kwa wakimbizi wa taifa kutafuta makazi kutokana na hofu ya uharibifu wa ustaarabu katika hilo taifa. Huku uhalifu ukiongezeka, mataifa hugeukia vita wakitafuta bidhaa. Ripoti ya mwaka 2015 inaashiria ya kwamba zaida ya theluji moja (1/3) ya watoto duniani wanakufa kila mwaka kutokana na utapia mlo (24). Marekani, moja kati ya watoto sita hulala njaa kila usiku (25,26). Mpango wa Chakula Duniani unabainisha ya kuwa: “Inatarajiwa kuwa watu milioni 345.2 watakuwa na uhaba wa chakula mwaka wa 2023 – mara mbili zaidi ya nambari iliyotarajiwa mwaka wa 2020. Hii inahususishwa na ongezeko kubwa ya watu milioni 200 ikilinganishwa na viwango kabla ya COVID-19. Zaidi ya watu 90,000 duniani wanapambana kuishi wakati wa njaa. Hii ni mara kumi zaidi kuliko ilivyokuwa miaka mitano iliyopita.” (26a)

Ili waweza kupata ajira, wakulima wanalima ardhi na wanafuga mifugo kwa shamba yao kupita kiasi. Hii inasababisha mmomonyoko wa udongo na kuenea kwa jangwa. Ardhi nyingine inachukuliwa ili itumiwe kwa makazi, uchimbaji madini, ukataji miti, ukulima, mibwawa ya maji (kwa hifadhi ya samaki), jambo ambalo linaangamiza aina za wanyama pori na mimea (27) na kulazimisha uhamiaji wa watu wengi (28).

Wataalam walithibitisha ya kwamba dunia inaweza kukimu karibu watu bilioni 6.2. Tumepitisha hii nambari, kama ambavyo kufa kwa binadamu 2% kwa miaka 15 iliyopita inathibitisha (29,29a). Licha ya hayo, idadi ya watu inaendelea kuwa kubwa. Tusipotatua mashida haya, hali itazidi kuwa ngumu na wakati unadidimia.

Ripoti za Umoja wa Mataifa zinaashiria ya kuwa tangu miaka ya 1990, karibu 50% ya wale walioishi kwa chini ya USD $1 kwa siku wanaishi kwa kiwango juu ya hii kiasi cha pesa sasa, kwa hisani ya juhudi za kuelekeza mgawanyo sawa wa mali na elimu, juhudi hizi zilizokuzwa na Umoja wa Mataifa, serikali nyingi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali. Kutokana na ongezeko kubwa la watu, nambari asili ya watu maskini haijapungua. Benki ya Dunia inaelezea jambo hili: “Ingawa kiwango cha ukuaji wa idadi ya watu ya nchi zinazoendelea imekuwa ikipungua kwa miongo kadhaa, idadi ya watu imeongezeka zaidi ya wale waliomo kila mwaka. Idadi hii kuongezeka imesababishwa na idadi msingi ya watu kuwa kubwa.” (30).Ongezeko hili imeonekana katika tabaka la kati, inasababisha ulaji, na hivyo kuzidisha uharibifu wa mazingira, na kukosa kuwezesha wakati wa maandhari kujaza na kustawii (31). Hii utajiri mpya inaonekana kwa ladha inayoongezeka ya matumizi ya vyakula visivyo sindika na ya wanyama. Kukidhi mahitaji ya bidhaa ya wanyama, ufugaji unatumia 40% ya ardhi duniani na 60% ya nafaka za kulisha mifugo (kuku, samaki, wanakondoo, mbuzi n.k.); biashara ya kilimo, inatumia 70% ya maji safi yanayopatikana (32) . Watu maskini wanatengwa kwa biashara ya kilimo kwa sababu ni faida zaidi kulisha mifugo kuliko kulisha watu maskini. Maendeleo ya kisayansi inayoangazia uzalishaji wa chakula, biashara ya kilimo imekua na kwa sasa imesababisha 50% ya ongezeko la joto duniani (33).

Chakula Kizima, Lishe Inayotegemea Mimea Hulinda Afya ya Binadamu Mali na Mazingira ( 33a ,33b )

Kulingana na Shirika la Afya Ulimwenguni, lishe inayotegemea wanyama ya: nyama ya wanyama, samaki na vyakula vingine vya baharini, mayai na maziwa inasababisha 63% ya maafa katika dunia iliyoendelea (34). 90% ya hizi kesi: ugonjwa wa moyo, kiharusi na saratani, aina ya pili ya ugonjwa wa bolisukari, ugonjwa autoimmune na Ugonjwa wa Alzheimer zinahusishwa moja kwa moja na bidhaa ya wanyama na vyakula vya kusindika (34g)

Mageuzi ya binadamu inaashiria ya kwamba binadamu kwa njia kubwa ni walaji wa mimea (34a, 34a1) na biokemia ya binadamu bado haijabadilika kwa namna ya kuweza kukabiliana na lishe ya wanyama, jambo ambalo linaloeleza viwango vya juu ya magonjwa na vifo vya binadamu (34b, 34c). Ushahidi wa kupungua mwendo wa mabadiliko ya mageuzi ni kwa mfano, wakati ambapo wagonjwa wanapopata magonjwa yaliyosababishwa na vyakula kama ugonjwa wa moyo, na wakose kula vyakula vyenye lishe ya wanyama (kama maziwa, samaki, mayai) na chakula cha kusindika, wanarudi sawa na wanapona (34d, 34e, 34f).Magonjwa haya yanayohusiana na vyakula au lishe yanasababisha athari kubwa kwa gharama ya huduma ya afya na tija.

Kwa mfano, katika mwaka wa 2014, gharama za kibinafsi na za serikali kwa huduma za afya Marekani zilikuwa mara tano zaidi ya gharama zake za kijeshi (35,35a,35b, 35c). Suluhisho ni rahisi: badilisha menyu iwe nafaka zisizochakatwa, matunda, kunde, mizizi, na mboga. Wakifanya hivyo, athari ya uponyaji kwa afya ya mtu itathibitishwa kwa muda isiyokuwa chini ya miaka miwili (36,37,37A)
Pata SUBTITLES chini ya video bonyeza CC, kisha bonyeza, , hapo bofya SUBTITLES , kisha, ⚙ tembeza na ubofye Kiswahili

Kumbukumbu ya filamu, “GAME CHANGERS’ inathibitisha kuwa walio na afya na nguvu zaidi ndio wenye hula mimea nzima, lishe wa aina isiochakatwa. Kuboresha afya yao, Arnold Schwarzenegger, mshindi wa cheo, Mr. Universe n.k. na gavana wa mji wa California, na Rais Bill Clinton walifuata mtindo huu mpya yenye afya.

Ongezeko ya Idadi ya Watu, Lishe Isiyofaa na Ulaji Huleta Madhara

Idadi ya watu inayoongezeka inazidisha uchafuzi, kutia kemikali iliyo na sumu shambani, anga, na maji, huku ikiangamiza kiini cha maisha. Hii inasababisha ongezeko la joto duniani, jambo ambalo linazidisha mafuriko, ukame, maporomoko ya matope, moto wa misitu na dhoruba n.k. Matukio haya yanasababisha jangwa, uyeyushaji wa barafu, kupanda kwa viwango vya bahari, na kuteketeza usambazaji wa maji safi, kwa kasi na kwa kiasi ambacho husababisha matokeo yasiyoweza kurekebishwa tusipochukua hatua ya kuyakomesha sasa.

TTuna ujuzi na fedha. Suluhisho hili linahitaji ushirikiano duniani, la sivyo, juhudi ya watu wachache hazitafaulu. Ni muhimu tuwezeshe wanawake wapate elimu, ujuzi wa kupanga uzazi na kupata namna tofauti wa kupanga uzazi, kufuata kanuni za maadili na za kibinafsi za kidini, ili wasihitaji kutafuta njia za kutoa mimba, kwa sababu kuzuia ni bora kuliko mambo yote (37a)Kupiga marufuku kwa njia halali ya kutoa mimba inaongeza viwango vya vifo vya uzazi, jambo linalotenga yatima na kuwawacha nyuma (37b)

Kwa kila $1, serikali inatumia kwa njia za kuzuia mimba, $7 inahifadhiwa(38) Tunafaa kupa ruzuku njia za kupanga uzazi kutumia mfano wa Thailand. Bado tuna uwezo wa kufikia mustakabali endelevu tukihakikisha ya kwamba kila familia mpya waelemishwe kuhusu jambo hili muhimu (38a). Huko Thailand, kutumia elimu na ruzuku, njia ya kupanga uzazi ilikubaliwa na kutekelezwa. Hii ilibadilisha uchumi, mazingira, na elimu yao sana mpaka kwa muda wa miaka tano, Bloomberg ilikabidhi Thailand cheo cha “Nchi Yenye Furaha Zaidi Duniani”(38b).

Tazama namna Thailand, bila kulazimishwa, ilitimiza hili lengo: (38c) Pata SUBTITLES chini ya video bonyeza CC, kisha bonyeza, , hapo bofya SUBTITLES , kisha, ⚙ tembeza na ubofye Kiswahili

Ulaji na kanuni za benki zisizokuwa na sera za maendeleo zimezorotesha maisha ya watu kifedha, mashirika na mataifa (Nchi za Ugiriki na Iceland ni mifano hapa) (39).Mapato ya usawa, kodi za ongezeko la thamani, kanuni za haki za benki na kuzuia mashirika kupata hadhi kama watu, inahitajika ili waweze kukomesha kuporomoka kwa uchumi, kuwezesha athari chanya katika usambazaji wa mali na njia ya matumizi ya fedha (40, 41).Tunafaa kukomesha ruzuku ya vyanzo vya sumu vya chakula, vyanzo vya sumu vya nishati. Sisi, kama Thailand, tunafaa kuweka ruzuku kwa njia za mpango wa uzazi. Tunafaa kuhimiza nguvu mbadala iliyo safi. Lazima tujifunze kuwa wasimamizi wazuri wa ardhi, ambayo itahitaji kutathmini bidhaa kwa kuzingatia gharama halisi ya kuzalisha na kuzitoa kutoka kwa mazingira yetu kulingana na athari za uharibifu wa mazingira na matatizo ya afya ambayo yanahusisha. Zaidi ya yote, tunapaswa kujifunza kuishi kwa kihafidhina. Utekelezaji wa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) utakatisha tamaa ya kuchafuka na kuchafua, kuzuia maisha yasiyo endelevu.

Hitimisho

Sasa tunajua ya kuwa hatuna wakati wa kupoteza. Tunajua kile tunachopaswa kufanya na kufanya hivyo kwa haraka.

Ukuaji wa idadi ya watu inaharibu maliasili, inabadilisha mifumo ya hali ya hewa, na inasababisha kutoweka kwa wingi wa mimea na wanyama, jambo ambalo si endelevu kwa wote. Kwa kufanya hivyo, hii inahatarisha uhai wa binadamu na uhai wote kwenye dunia yetu dhaifu. Njaa inayotokana na uharibifu wa mandhari inasababisha kuongezeka kwa utumizi wa madawa ya kulevya, uhalifu, ukosefu wa makazi, kupigana wa kijamii, chuki dhidi ya binadamu, na ubaguzi wa rangi inayokomesha maelewano na amani. Pamoja na elimu na upangaji wa uzazi, riziki na urejesho wa mazingira yaliyopotea inaweza kutimizwa (42) Kubadilisha lishe yetu ya mimea mzima, vyakula ambavyo havijasindikwa vitaboresha afya yetu na kutupa fedha ili tuhitimu: huduma ya afya kwa wote, elimu, kurejesha mfumo wa ikolojia, utafiti kwa ajili ya kurekebisha na kuunda teknolojia ya ufanisi itakayomaliza uharibifu wa mazingira. Tukizingatia haya, tutapata wakati wa kuhakikisha kwamba binadamu watafuata njia ya uendelevu na amani.

Kwa kuwezesha watu wetu wapate kazi badala ya kutumia vifaa, tutaweza kuboresha hali yenye binadamu huishi na kurejesha utu wa binadamu. Kwa kubadilisha dhana, tutapata nafasi ya kurejesha hisia za jumuiya na maelewano. Kwa kuhamasisha amani, fedha za kijeshi zitatolewa kwa ajili ya maendeleo ya wote (43,44).

Tunapoangazia ulimwengu usio na mwisho, tunajua ya kuwa dunia ndio pahali pekee panapoweza kutukimu. Bahari za matatizo imepeleka chombo chetu dhaifu mahala ambapo tumeelewa ya kuwa tukiwa pamoja, ndivyo tutaweza kuokoa hazina kuu kuliko yote – maisha yenyewe. Tunajifunza ya kuwa tukiwa pamoja kama familia duniani, tutaweza kuwapisha kizazi kipya tochi ya maisha. Njia hii itahitaji kuacha nyuma ubinafsi, siasa na tamaa. Tukibadili mienendo yetu na kuheshimu yote yaliyoumbwa na Mungu, kizazi kipya itarithi dunia ambayo nyimbo ya ndege za mwituni na marashi yaliyotokana na maua ya msitu inatupa furaha kwa mioyo yao, mahali ambapo watapaita NYUMBANI(45) mahali ambapo wote wanaweza ishi kwa heshima na amani.

*Benki kuu ya Dunia inaeleza umaskini wa wastani kuwa: kuishi kwa $1 - $2 kwa siku

**Ufafanuzi wa Tume ya Dunia ya Mazingira inaeleza neno endelevu kuwa: Jamii endelevu ni jamii mojawapo iliyo “timiza mahitaji ya sasa bila kuafikiana na uwezo wa kizazi ijayo kutimiza mahitaji yao wenyewe.

Dr. Gabriela Kaplan, M.D. (C) 2023
Imerekebishwa 2023

clickmore

Maoni KuHusu Kazi Yetu

Norman E. Borlaug - mshindi wa Tuzo la Amani la Nobel la mwaka wa 1970. Nakubaliana nawe kabisa ya kwamba watu wengi mno ni chanzo cha njaa, uhalifu, madawa ya kulevya, ukosefu wa ajira, utengano wa kifamilia na madhara makubwa kwa mazingira ... Nimejaribu kuhamasisha dunia kuhusu 'dubwana la idadi ya watu,' Nilivyosema tatizo hili wakati mimi akitegemea kupokea Tuzo ya Nobel Nakupongeza sana kwa makala hii nzuri. Ni makala iliyo kina, ya kweli na pana sana ambayo nilipokea kuhusu mifululizo hii tata ya masuala yanayohusiana ambayo yataathiri mustakabali wa ustaarabu.
Linus Pauling - mshindi wa Tuzo la Amani la Nobel la mwaka wa 1962. It ni nzuri sana kuona wewe kusema tatizo la kuwa na watu wengi mno. ni nzuri sana kuona kwamba we tatizo la watu wengi mno …Niliandika kitabu miaka iliyopita ambayo kimsingi kilikuwa kinahusu tatizo la idadi ya watu, na nimendelea kufanya kazi katika masuala haya ya idadi ya watu.
Mtakatifu Teresa wa Calcutta - mshindi wa Tuzo la Amani la Nobel mwaka wa 1997. Kupitia kazi hii ya moyo wako tunaomba ya kwamba utakatifu wako uendelee kuongezeka.
Vigdis Finnbogadottir, Rais wa Iceland. Ingawa Iceland ni moja ya mataifa machache duniani ambapo idadi kubwa ya watu si tatizo, tunafahamu tishio lililoko la idadi kubwa mno ya watu kwa mazingira ya kimataifa, hasa tunapozungumzia kuhusu suala la utupaji takabaharini, kwani samaki ndio riziki yetu kuu.
George Vassiliou, Rais wa Cyprus. Ni ukweli ya kwamba idadi kubwa mno ya watu imekuwa suala la kimataifa na kwamba na ni lazima hatua ya pamoja ichukuliwe na nchi zote ilikuhakikisha kuwepo kwa mazingira bora kabisa ya maisha katika sayari hii.
Ricardo Arias Calderón, Makamu wa Rais wa Panama. Nakutumia nakala ya ripoti yako. 'Fumbuzi za Kiutendaji kwa Matatizo yaliyosababishiwa na idadi kubwa mno ya watu' kwa taasisi zote za serikali zinazoshughulikia mada hii katika nchi yangu.
Corazon Aquino, Rais wa Philippines. Ni lazima tufanye kila kitu kadri ya uwezo wetu ili kukabiliana na masuala ya kimataifa ya idadi kubwa mno ya watu. Masuala haya yanavuka mipaka ya kijiografia na hivyo basi yanahitaji tahadhari ya watu kila mahali.
Amata Kabua, Rais wa Visiwa vya Marshall. Nimetazama tatizo hili kwa tishio sawa kama wewe, kwani eneo la nchi ya taifa langu la kisiwa ni ndogo kabisa na yenye mipaka, na kwa wakati huu idadi ya watu wetu ni kubwa mno katika historia ya nchi yetu.
Bill Clinton, Rais wa Marekani. Suala hili la idadi kubwa mno ya watu ni jambo muhimu ambayo kwa hakika linahitaji kutathminiwa. Nimetuma barua yako kwa Mpasuaji Mkuu Marekani, Dk Joycelyn Elders.
Mchungaji Desmond M. Tutu - mshindi wa Tuzo la Amani la Nobel la mwaka wa 1984. Nimependezwa sana na somo hili lakini tatizo la mlipuko wa idadi ya watu imejaa na matatizo makubwa ya kisiasa, kama vile hapa nchini Afrika Kusini.
Al Gore Jr. - mshindi wa Tuzo la Amani la Nobel la Mwaka wa 2007. Ninafahamu kuwepo kwa uhusiano msingi na muhimu kati ya ongezeko la kasi la idadi ya watu na ongezeko la dhiki ya mazingira, na ninakuhakikishia ya kwamba nitaendelea kufanya kazi huku nikizingatia swala hili kwa karibu.
Baba Mtakatifu, Papa Yohane Paulo II. Sekretarieti wa Taifa la Vatican Mtakatifu Papa Yohane Paulo II amenielekeza kushiriki ujumbe ufuatayo - Crescenzio Sepe: Holy See inatambua jukumu na wajibu linalohitajika ilikukabiliana na tatizo hili la idadi ya watu. Holy See inazingatia vidokezi vya ukuaji wa idadi ya watu kwa mustakabali wa familia ya binadamu ... ya kwamba kuna haja ya kuunda jumuiya ya kimataifa iliyo na ahadi ya 'kufanya maisha imfae binadamu zaidi' kwa maadili yote ya kiroho ili kuwawezesha watu kuona hasira halisi ya vitu vya kimwili , bila kudhabihu maadili mengine. Mapendekezo, kwa kweli, yanataja jukumu isiyofidika ya familia kama 'msingi wa jamii'.

BOARD MEMBERS

Dr. Gabriela Kaplan, MD, President Medical Doctor, Neuroradiology and Imaging, (USA)
Dr. Ada Contreras MD Medical Doctor, Pediatric Neonatologist, (Honduras)
Sta. Nalda Bustamante  Ministerio de Educacion, U.N.F.P.A., technical Advisor, (Ecuador)
Dr. Benjamin Gentin, MD  Medical Doctor, Internal Medicine, (South Africa)
Dr . Charles Grace, Esq.  Engineer, Intellectual Property Attorney  (USA)
Mrs Vilhelmina Sluvko Govt. Dept. of Health-Environment, Senior Specialist, (Latvia)
Fr.  Joseph Rinaldo, Sdc. Servants of Charity, Provincial   ( Italy)
Dr.  Araceli Aulestia, DDS DDS, I.N.S.T.R.A.W.,U.N. for Entity for Gender Equality (Ecuador)
Dr. Javier Vasquez, MD   Medical Doctor, Pediatric Psychiatry, (Peru)
Mrs. Sylvia Wachner Business Administration, Project Manager,  Organic Agriculture, (Brazil)

ADVISORS

Fr.Stanislaw Chapievski, S.J.   Education, Polapoland Tatrzanaka Gdyaiand, (Poland)
Prof. Jean Claude Kaplan, MD       Medical Doctor, Molecular biology-biochemistry I.N.S.R.M.,(France)
Mr. Josphat Ngonyo                   Director Africa Network Animal Welfare, UN FAO Editor,Wildlife  (Kenya)
Dr. David Pimentel, Ph.D           Ecology, Entomology. Cornell University ,(USA)
Dr. Bill Ryerson              Biologist.  Post Carbon Fellow, Yale University, (USA)
 

Gabriela D. Kaplan, MD, alikabidhiwa tuzo ya Albert Nelson Marquis Lifetime Achievement Award na Marquis Who's Who http://gabrielakaplanmd.lifewatchgroup.org/
https://lifewatchgroup.com/


mkutano lifewatchgroup

To COMMENT: Enter your Zip code or use Zip enclosed. to send your comments to media, state, local! enter zip code find your reps.

Tafuta majibu yako lifewatchgroup


FOR FURTHER READING AND NEWS:

Brookings Institute. Climate and Energy Economics https://www.brookings.edu/blog/planetpolicy/2018/04/21/why-the-climate-challenge-needs-congressional-action/
Center for Nutrition Studies http://nutritionstudies.org/
CONDOMS: From Poverty to Prosperity with
Dr. Viravaidya
http://www.lifewatchgroup.org/37a/index.html
Emergency Contraception Princeton University http://ec.princeton.edu/questions/ectime.html
Family Planning Couple to Couple League up http:// ccli.org
Global Network of Science Academies IAP http://www.interacademies.org/
International Atomic Energy Agency https://www.iaea.org/
Johns Hopkins University. Hopkins Population Center http://web.jhu.edu/popcenter
Preventing Infant Mortality - La Leche League http://www.llli.org/
World Census Bureau www.census.gov/
World Resources Institute: Equity, Prosperity http://www.wri.org/
W. Smith, Restoring Forests http://www.ted.com/talks/willie_smits_restores_a_rainforest?language=en
REVISED 2023 | www.lifewatchgroup.org